Wednesday, November 29, 2017

SIMULIZI ZA KWELI - #1 Jesu Dasi, Mmisheni wa Injili kwa Asia (GFA)


Mmisheni Jesu Dasi aliogopa alipotembelea kwa mara ya kwanza kijiji kimoja na kukuta hakuna waamini pale. Watu wote walikuwa wakiabudu mamia ya miungu mbalimbali, na makuhani wanne waliwatawala na kuwaendesha kupitia uchawi wao.

Hadithi zilisimuliwa jinsi ambavyo makuhani hawa walivyoweza kuua mifugo ya watu na kuharibu mazao yao. Watu waliugua ghafla na kufa bila maelezo. Uharibifu na vifungo ambavyo wanakijiji hawa waliishi chini yake ni vigumu hata kuvifikiria. Majeraha, uharibifu na kifo vilikuwa dhahiri katika nyuso zao, kwa sababu walitawaliwa na kuendeshwa na nguvu za giza.

Jesu Dasi alipowaambia habari za Kristo, ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuna Mungu ambaye hakuhitaji sadaka na matoleo ili kutuliza hasira Yake. Kadri Jesu Dasi alivyozidi kuhubiri masokoni, watu wengi walimpokea Bwana Yesu kama Mwokozi wao.

Lakini wale makuhani waligadhabishwa sana. Walimuonya Jesu Dasi kuwa asipoondoka katika kijiji chao basi wataiita miungu yao ili imuangamize yey, mke wake na watoto wao. Jesu Dasi hakuondoka. Alizidi kuhubiri, na wanakijiji wakazidi kuokolewa.

Mwishowe, baada ya wiki chache, wale wachawi wakaja kwa Jesu Dasi na kumuuliza siri ya nguvu zake.

“Hii ni mara ya kwanza nguvu zetu zimeshindwa kufanya kazi,” walimwambia. “Baada ya kufanya puja zote tukaziamuru mizimu ziende na kuiua familia yako. Lakini mizimu ilirudi na kutuambia kuwa hawakuweza kuisogelea familia yako wala wewe mwenyewe kwa kuwa mlikuwa kila mara mmezungukwa na moto. Basi tukaziita mizimu yenye nguvu zaidi ili zikudhuru – Lakini nayo ikarudi, ikisema kuwa siyo tu kuwa ulikuwa umezungukwa na moto, lakini pia Malaika walikua wakikuzunguka muda wote.

Jesu Dasi aliwaambia hbari za Kristo. Roho Mtakatifu akawagusa juu ya hatia ya dhambi zao kila mmoja, dhambi ya kuyafuata mapepo na juu ya hukumu inayokuja. Kwa machozi, wakatubu na kumpokea Yesu Kristo awe Bwana wao. Kwa sababu hiyo, mamia ya wanakijiji wengine, wakawekwa huru kutoka katika dhambi na vifungo vyao.

Mwisho.

Je unateswa na Shetani na mawakala wake? Yesu ndio kimbilio. Wasiliana nasi kwa anuani kulia kwa andiko hili au inbox ya facebook.

Mistari ya kutafakari:
Je, nina maana kwamba kafara iliyotolewa kwa sanamu ni kitu chenye maana yo yote? Au kwamba sanamu ni kitu chenye maana yo yote? La hasha! Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani” 1Wakorintho 10:19-20
Oneni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe watoto wa Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini ulimwengu haututambui, ni kwa kuwa haukumtambua… Lakini mwajua ya kuwa Yeye alidhihirishwa ili aziondoe dhambi… Yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa sababu Ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize kazi za Ibilisi”. 1 Yohana 3: 1-8
(Imetafsiriwa toka katika kitabu kiitwacho “Revolution in World Missions” uk. 21-22). Tafadhali pitia mtandao wao http://gfa.org