Mmisheni Jesu Dasi
aliogopa alipotembelea kwa mara ya kwanza kijiji kimoja na kukuta
hakuna waamini pale. Watu wote walikuwa wakiabudu mamia ya miungu
mbalimbali, na makuhani wanne waliwatawala na kuwaendesha kupitia
uchawi wao.
Hadithi zilisimuliwa
jinsi ambavyo makuhani hawa walivyoweza kuua mifugo ya watu na
kuharibu mazao yao. Watu waliugua ghafla na kufa bila maelezo.
Uharibifu na vifungo ambavyo wanakijiji hawa waliishi chini yake ni
vigumu hata kuvifikiria. Majeraha, uharibifu na kifo vilikuwa dhahiri
katika nyuso zao, kwa sababu walitawaliwa na kuendeshwa na nguvu za
giza.
Jesu Dasi
alipowaambia habari za Kristo, ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuna
Mungu ambaye hakuhitaji sadaka na matoleo ili kutuliza hasira Yake.
Kadri Jesu Dasi alivyozidi kuhubiri masokoni, watu wengi walimpokea
Bwana Yesu kama Mwokozi wao.
Lakini wale makuhani
waligadhabishwa sana. Walimuonya Jesu Dasi kuwa asipoondoka katika
kijiji chao basi wataiita miungu yao ili imuangamize yey, mke wake na
watoto wao. Jesu Dasi hakuondoka. Alizidi kuhubiri, na wanakijiji
wakazidi kuokolewa.
Mwishowe, baada ya
wiki chache, wale wachawi wakaja kwa Jesu Dasi na kumuuliza siri ya
nguvu zake.
“Hii ni mara ya
kwanza nguvu zetu zimeshindwa kufanya kazi,” walimwambia. “Baada
ya kufanya puja zote
tukaziamuru mizimu ziende na kuiua familia yako. Lakini mizimu
ilirudi na kutuambia kuwa hawakuweza kuisogelea familia yako wala
wewe mwenyewe kwa kuwa mlikuwa kila mara mmezungukwa na moto. Basi
tukaziita mizimu yenye nguvu zaidi ili zikudhuru – Lakini nayo
ikarudi, ikisema kuwa siyo tu kuwa ulikuwa umezungukwa na moto,
lakini pia Malaika walikua
wakikuzunguka muda wote.
Jesu
Dasi aliwaambia hbari za Kristo. Roho Mtakatifu akawagusa juu ya
hatia ya dhambi zao kila mmoja, dhambi ya kuyafuata mapepo na juu ya
hukumu inayokuja. Kwa machozi, wakatubu na kumpokea Yesu Kristo awe
Bwana wao. Kwa sababu hiyo, mamia ya wanakijiji wengine, wakawekwa
huru kutoka katika dhambi na vifungo vyao.
Mwisho.
Je unateswa na Shetani na mawakala wake? Yesu ndio kimbilio. Wasiliana nasi kwa anuani kulia kwa andiko hili au inbox ya facebook.
Mistari
ya kutafakari:
“Je,
nina maana kwamba kafara iliyotolewa kwa sanamu ni kitu chenye maana
yo yote? Au kwamba sanamu ni kitu chenye maana yo yote? La hasha!
Lakini kafara za watu wasiomjua Mungu hutolewa kwa mashetani, wala si
kwa Mungu. Nami sitaki ninyi mwe na ushirika na mashetani”
1Wakorintho 10:19-20
“Oneni
ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe watoto wa
Mungu! Nasi ndivyo tulivyo. Sababu kwa nini ulimwengu haututambui, ni
kwa kuwa haukumtambua… Lakini mwajua ya kuwa Yeye alidhihirishwa
ili aziondoe dhambi… Yeye atendaye dhambi ni wa Ibilisi, kwa sababu
Ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana
wa Mungu alidhihirishwa ili aziangamize kazi za Ibilisi”. 1 Yohana
3: 1-8
(Imetafsiriwa
toka katika kitabu kiitwacho “Revolution in World Missions” uk.
21-22). Tafadhali pitia mtandao wao http://gfa.org
No comments:
Post a Comment