Yesu Kristo

Mara ya Mwisho Dunia kumwona Yesu ilikuwa msalabani, akining'inia kwa aibu. Ni kipindi alipokuwa akipigwa makofi na kutemewa mate. Yesu ambaye dunia inamjua ni Yesu mnyonge kama kondoo anayepelekwa machinjioni! Bahati mbaya kwao, wanaendelea kufikiri kuwa Yesu bado yupo kama kondoo.

Yesu Kristo alimaliza kazi kama mwanakondoo wa Mungu na kufufuka kama Simba wa Yuda! Yesu alikiwisha urudia utukufu wake wa Kwanza aliokuwa nao Pamoja na Baba na Roho Mtakatifu. Na ndipo sasa Yohana, ambaye alikaa katika kifua cha Yesu kama Mwanafunzi mpendwa alipokutana na Simba Huyu anayetisha kwa utukufu na uweza na mamlaka wa Yuda hichi ndicho alochoandika:
Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. (Ufunuo 1:7)
Yesu atakaporudi kama Simba wa Yuda, ulimwengu hautaamini unachokiona. Maana walimtukana na kumdhihaki na kumsema vibaya na sasa anarudi kwa utukufu kama Mungu mwenye nguvu na Mfalme wa wafalme. Wataomboleza lakini haitawasaidia! Si hivyo tu, lipo baya zaidi ya hilo.

Yesu atakaporudi, na baada ya ile miaka elfu ya raha duniani kwisha, kitawekwa kiti cha enzi cha hukumu naye ataketi awahukumu wafu na walio hai sawasawa na matendo yao. Waliowahi kuiba na kudanganya na kutamani na wengine wote waliovunja amri za Mungu watahukumiwa katika ziwa la moto liwakalo na kiberiti (sulfur).

Habari njema ni kuwa deni lako linaweza kulipwa kama utatubu na kugeuka na kuacha njia zako mbaya na kumlilia Yesu akuokoe na kukusafisha kwa damu yake. Hapo utaokoka na siku ile ya kutisha itakayomjilia kila mwanadamu aliyewahi kuishi duniani.

Chagua kukutana na Yesu kama rafiki au kama Jaji wa ulimwengu ujao punde, Mbingu au Jehanamu ya Moto, Kufurahi na Mungu milele au Jehanamu mbali na uzuri na wema wa Mungu unaoufurahia leo n ujao. Chaguo ni lako, ila nakushauri uchague Mfalme Yesu ili upate kuishi. Kumbuka :
"yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam."
Amina.

~ Stefano D. Mtangoo